Mungu wa miujiza by mercy wairegi wedding

Mungu, Unabii, na Maarifa ya Miujiza

Misc.

Mtu mwenye moyo myoofu ambaye anakuja kutambua kuwepo kwa Mungu na kutafakari asili yake ya ajabu hawezi kujizuia kustaajabia ujuzi wake wa kujua yote. Kama mtunga Zaburi anavyodai,

“Ee Bwana umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote. Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa, BWANA. Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda Mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko”(139:1-4, 6-8).

Biblia hutaarifu kwamba Mungu “anazijua siri za moyo” (Zaburi 44:21), kwamba macho Yake “yako kila mahali” (Mithali 15:3), na kwamba “ufahamu wake hauna kikomo” (Zaburi 147:5). Kwa ufupi Mungu “anajua mambo yote” (1 Yohana 3:20). Ana ujuzi kamili wa wakati uliopita, wa sasa, na hata wakati ujao. Ayubu alikuwa sahihi kuuliza swali la kiajabu, “Je, kuna yeyote anayeweza kumfundisha Mungu ujuzi?” (21:22).

Je, Kuna Uwezekano Mwingine?

Huenda wengine wakafikiri kwamba mwandishi wa Biblia anayefanya uaguzi wa kipagani angeweza pia kuandika kwa usahihi mambo ambayo yangetokea wakati ujao wa mbali (Katika Tiro, Babiloni, Yerusalemu, n.k) kwa sababu shetani au kiumbe Fulani cha roho mwovu alimfunulia habari hizo. Hitimisho kama hilo, hata hivyo, haikubaliki kwa sababu kadhaa:

  • Kwanza manabii walishutumu kila aina ya uchawi, ikijumuisha uaguzi na ubashiri (Kumbukumbu la Torati 18:9-14; Yeremia 27: 9-29:9). Kwa hiyo, wangekuwa wanajihukumu wenyewe ikiwa kweli walikuwa wapiga ramli.
  • Pili, kwa kuwa Mungu, kwa ufafanuzi wake hasa, ndiye pekee anayejua yote, Mwenye uwezo wote (1 Yohana 4:4), si shetani aliyeumbwa na kuanguka wala kiumbe mwingine yeyote asiye wa milele (Wakolosai 1:16; 2 Petro 2:4) anaweza kuchagua kujua chochote anachotaka. Anaweza kupata ujuzi upesi kutoka kwa viumbe wengine au kutokana na uzoefu wa kibinafsi, lakini hatimaye, roho waovu wanaweza tu kuwa na ujuzi wa kile ambacho Muumba anawaruhusu kujua (1 Wakorintho 2:11). Kwa kielelezo, ikiwa kiumbe-roho mwovu angejua matukio ya wakati ujao, ingelikuwa ni kwa sababu ya mtawala wa mbingu na dunia anayejua yote kumpa ujuzi huo kwa makusudi Yake mwenyewe. “Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza? (Maombolezo3:37). Kwa ufupi, hakuna mtu anayetabiri kwa usahihi wakati ujao isipokuwa Mungu amjulishe juu yake.

[KUMBUKA: Waaguzi wanaweza kutabiri mara kwa mara na kwa njia isiyo wazi jambo litakalotokea, lakini ubashiri kama huo au utabiri wa hali ya hewa uko mbali na ufunuo, ujuzi wa kimbele wa Mungu usio wa kawaida, ambao ulifunuliwa nyakati za Biblia kwa wasemaji wake wa kweli.]

  • Tatu, Mungu alifunua katika Maandiko yote kwamba wale wanaotabiri kwa usahihi wakati ujao ni manabii halisi wa Mungu. Yeremia aliandika hivi: “Nabii atabiriye habari za Amani, neno la nabii yule litakapotokea, ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa BWANA amemtuma kweli kweli” (Yeremia 28:9). Kwa upande mwingine, wale wanaotabiri mambo ambayo hayatatimia, “Bwana hakuwatuma, wanatabiri uwongo” (Yeremia 28:15; 29:8-9). “Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena BWANA? Atakapo nena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope”(Kumbukumbu la Torati 18:21-22). Ikiwa waaguzi wasioongozwa na roho ya Mungu wangeweza kutabiri wakati ujao kwa nguvu za kiumbe Fulani mwovu, basi mtu mwenye moyo mnyoofu angewezaje kujua kwa hakika nini na ni nani wa kuamini na kutii? Kukata kauli kwamba waaguzi wa kipagani wamepewa nguvu na roho waovu ili kutabiri wakati ujao bila dosari, kunapingana na yale ambayo manabii wa kweli walioongozwa na roho ya Mungu walifundisha, na kuwazuia wanaotafuta ukweli wasiweze kujua kweli.

Hitimisho

Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayejua yote, Mwenye uwezo wote. Yeye pekee ndiye anayejua kila kitu- hatimaye, Yeye peke yake ndiye anayejua siku zijazo-ufunuo wa mawazo hayo ya kiungu kuwa moja wapo ya njia kuu ambazo mwanadamu amehitimisha kimantiki kwamba ujumbe fulani kwa hakika uliongozwa na Mungu. Inaonekana kuwa hatari sana kukata kauli kwamba viumbe-“roho walioanguka” wanajua wakati ujao na wamefunua habari hizo za kimuujiza kwa waaguzi waovu. Ndiyo, watabiri ambao hawakuongozwa na roho bila shaka wamejaribiwa na kusukumwa katika vizazi vyote na nguvu zenye nguvu za giza, lakini viumbe hao ni “roho zidanganyazo” zisizo na ujuzi wowote (1 Timotheo 4:1), ambazo humfuata “baba yao, Ibilisi,” “mwongo” ambaye “hakuna ukweli ndani yake” (Yohana 8:44).

Ilichapishwa awali katika Gospel Advocate, Machi 2015, 157[3]:27-28.

Rejea

Butt, Kyle and Dan Barker (2009), Does the God of the Bible Exist? (Montgomery, AL: Apologetics  Press).


Published

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→